TANZANIA: Je, Jux anawasiliana na Jackie? Soma hapa kujua zaidi!
9 February 2016

Msanii wa muziki, Juma Jux amedai Jackie Cliff aliyedaiwa kukamatwa na madawa ya kulevya nchini China na kufungwa jela, yupo salama na amekuwa akiwasiliana naye.
Akizungumza na 255 katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumatatu hii anashindwa kuzungumzia vitu vingine vya ndani kwakuwa mrembo huyo hapendi.
“Huwa tunafanya mawasiliano ingawa sio mara kwa mara. She is okay, yuko sawa. Nimewasiliana nae kama miezi miwili hivi iliyopita. Siwezi kuongelea sana vitu vingine hata hivyo yeye mwenyewe huwa hapendi niwe naongea ongea na watu kuhusu maisha yake”, alisema Jux.
Aliongeza, “Kuhusu ndugu zake wanasikia. Kuna watu wake wa karibu. Pia kuna watu wengine wanaposikia sikia wanaweza kuona kama mimi nachukua advantage yake, kwasababu kila mtu ananiuliza vipi fulani vipi fulani, ndio maana muda mwingine anasema acha usiongee ongee”.




Leave your comment