TANZANIA: Si kweli tunapewa hela ili kupiga nyimbo za wasanii – B12
5 February 2016

Mtangazaji wa muda mrefu wa kipindi cha XXL cha Clouds FM, Hamis Mandi maarufu kama B-12 amesema sio kweli kwamba wanahongwa hela na wasanii ili wacheze nyimbo zao katika kipindi cha XXL.
Akizungumza katika kipndi cha Mkasi TV, B-12 alisema wanaogopa sana mtu anayekuja na hela ili wimbo wake uchezwe.
“To be honest tungekuwa tunapiga muziki alafu tunapewa hela, sidhani kama show yetu ingekuwa namba moja”, alisema. “Its true kuna watu wanakuja wana hela kabisa wanakwambia mimi nina kiasi kadhaa nataka unifanyie promotion. Lakini ukweli haupo hivyo, unajua unaponipa mimi hela yako ili nipige nyimbo yako, nitaipiga siku mbili halafu nitaipotezea”.
Aliongeza, “Sema to be honest hivyo vitu vipo. Lakini msanii mwenyewe inabidi ajue iwapo anatumia pesa kupromote muziki wake, ile ni kama biashara nyingine ambayo inategemea pesa ambayo umewekeza. Pia ogopa sana msanii ambae anatumia hela, wimbo wake unaweza ukawa haujafikia viwango ambavyo vinahitajika”.




Leave your comment