TANZANIA: Je unajua utafiti alioufanya Ben Pol nchi za Ulaya? Soma hapa kujua ni utafiti gani!
2 February 2016

Muimbaji wa muziki wa R&B, Ben Pol amesema mwezi Januari mwaka huu amefanya tour ya Ulaya ili kufanya utafiti wa muziki wake pamoja na kujifunza jinsi ya kupenyeza muziki wake!
Ben Pol amesema kuwa utafiti huo aliufanya katika nchi ya China, Malaysia pamoja na Qatar.
“Kikubwa mimi nilienda kufanya utafiti wa muziki wa Ulaya sana. Wanasikiliza muziki wa Uingereza hata wa Marekani hauchezwa kivile. Kwahiyo nimegundua nyimbo za club zile za kuchezeka, Rock na House ndio wanasikiliza sana”.
Pia Ben Pol ameongeza kuwa tour hiyo ameitumia kama sehemu ya mapumziko ya mwanzo wa mwaka baada ya kufanya kazi nyingi mwaka uliopita.
Bongo: Bongo 5




Leave your comment