TANZANIA: Sallam ataja majukum yake kwa Diamond kama meneja!

 

Mmmoja kati ya mameneja wa wa Diamond Platnumz, Sallam ameeleza majukumu yake akiwa kama meneja wa msanii huyo ambaye kwa sasa ana mafanikioa makubwa ya kimuziki Afrika.

Akiongea kwenye kipindi cha Swahili Talk Radio ya nchini Denmark, ingawa wote wamegawana majukumu lakini pia wanashirikiana katika maamuzi ya kila jambo.

“Hapa kuna meneja kuna business meneja yaani wote tunashirikiana katika kila suala ambalo linaletwa kama ajenda ‘Jamani mwaka huu 2016 tunafanyaje’ labda ajenda zipo 15, tunatakiwa tufanye tour, nyimbo tutoe ngapi na target yetu ni hii. Kwahiyo ni vitu ambavyo vyote vinawekwa juu ya meza na tunajadili” alisema.

Sikiliza zaidi hapa chini;

 

Leave your comment