TANZANIA: Vitu nane usivyovijua kuhusu Wema na Idris kabla na baada ya uhusiano wao!
29 January 2016

Baada ya mrembo Wema na mshindi wa Big Brother Africa 2014, Idris Sultan kuweka uhusiano wao wazi, vitu vingi vimekuwa vikisemwa kuhusu wapenzi hao.
Lakini leo tumekusogezea mambo nane ambayo huyajui kuhusu wapenzi hao jinsi gani walikutana kwa mara ya kwanza;
- 01-Walikutana vipi; Nilimfahamu Idriss akiwa anafanya kazi kwa Raqey, picha niliyopost jana kumtakia heri ya kuzaliwa ilikuwa picha ya kwanza kupiga mimi nayeye siku hiyo …Baadae nikamuona kwenye Big Brother, nilimpenda na nilipenda kumuangalia.. alivyorudi nikamtumia message Instagram akaniambia atanitafuta”- Alisema Wema.
- 02-Kilichofatia baada ya Idris kurudi – ‘Nilimwalika nyumbani kwangu, tukaongea na tukawa na mawasiliano ya karibu sana mpaka usiku wakati mwingine’ – Wema
- 03-Wema alivyochukulia ishu ya Samantha kuja TZ-‘Idris alimleta mpenzi wake waliyekutana kwenye Big Brother wakati tayari tulikuwa na uhusiano.. Nilivumilia nikijua Samantha hatokuwepo Tanzania muda wote’ – Wema.

Idriss akiwa na Samntha
- 04-Wema alivyokutana na Luis- ‘Kuna siku walikuja na Luis nikamtania Idris kwamba jamaa ni mzuri, sikusema nataka kulipiza kwasababu yeye yuko na Samantha japo iliniuma.. nilikutana na Luis kwenye Instagram Party tukaanza uhusiano kwasababu nilikuwa naumizwa pia kumuona Idris na Samantha’ – Wema.

- 05-Idris kuhusu mtoto – ‘Yes natarajia kupata mtoto wangu wa kwanza’ – Idris
- 06-Kilichomvuta Idris kwa Raqey ambako alikutana na Wema- ‘Nilichaguliwa kusomea udaktari nikaona huko hakutonifaa sana, nikaona nikafanye kazi kwa Raqey ambapo nilipata kazi nyingi za mabango’ – Idris
- 07-Mara ya kwanza Idris anavutiwa na Wema ilikuwa hivi – ‘Nilianza kufanya kazi za Wema, ilikuwa kila nikipata kazi ya picha za Wema nziangalia sana.. nilikuwa navutiwa nazo sana’ – Idris
- 08-Picha ya kwanza Idris alivyopiga na Wema – ‘Siku ya kwanza tunapiga picha tulikuwa kwenye location ya kushoot Wema akiwa amevaa majani majani.. ndio picha alivyopost jana’ – Idris
Wema na Idris waliyasema hayo kwenye kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM jana Alhamisi, kinachotangazwa na Diva The Bawse.




Leave your comment