EXCLUSIVE (TANZANIA) – Serikali ya Magufuli kuifungia Zari All White party kufanyika nchini (TZ)
18 January 2016

Serikali ya Magufuli yaifungia Party ya All White Party ya Zarina Hassan kwa madai kuwa alikiuka masharti ya Basata kwa mwaka 2014.
Baraza la Sanaa (BASATA), limedai kuwa mzazi mwenzake na Diamond amekiuka masharti kwa kuanza kutangaza kuhusu tukio hilo kabla ya kupata ruhusa kutoka kwenye baraza hilo.
Mbali na kumpa faini ya kutoa kiasi cha Tsh 483,000 (Kes 23,000) pia amekatazwa kuendesha party hiyo nchini Tanzania hadi atakapoweza kutimiza masharti yaliyowekwa.
Hadi sasa bado Zari hajaongelea suala hilo, pia tunaendelea kusikilizia jinsi itakavyokuwa kwa kipindi hichi cha uongozi wa Magufuli.




Leave your comment