EXCLUSIVE (TANZANIA) – Diamond kufunguka kuhusu mtoto wake mwingine huko Mwanza.
18 January 2016

Msanii Diamond Platnumz afunguka kuwa na mtoto mwingine na msichana waliyekutana kwa mara moja tu enzi wakati anaanza kuwa staa (one night stand) mbali na Tiffah aliyezaa na Zari.
Taarifa hizo zilitolewa hivi karibuni na Diamond mwenyewe wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Papaso cha TBC FM. Alisema tukio hilo lilitokea mwaka 2010, jijini Mwanza alikoenda kufanya show.
“Huyo mwanamke story ilivyokuwa ametoka chumba cha brother Dully akaja kwangu mimi nikafanya yangu, mimi nikarudi mtoto akawa ananiambia ‘ebwana mimi nina mimba’ alisimulia Diamond.
“Basi ilivyokuwa ‘ebwana eeh mimi nina mimba’ na mimi nikawa nachezesha nini nikawa namhudumia, huku na huku bahati mbaya nikaanza na demu fulani hivi kwahiyo demu mwenyewe akanimind, nikawa nampigia simu hapokei nikaenda Mwanza kumsakanya huku na huku nasikia kwao wakanimind nikaonekana kama mimi nazingua”, alisema.
“Siku moja nikaenda nikambanabana ‘nikamwambia wewe una mtoto’ akanikatalia kwasababu aliniambia ile mimba niliitoa nini, kumbe ni muongo. Nikaja nikamchunguza kumbe alikuwa amezaa na mtoto namuambia ‘nataka basi nimuone mwanangu’ alinikatalia sana lakini baadaye akaja akaniambia ni kweli ni mwanao na umefanana naye na nini. Nikamwambia naomba nimuone kwenye picha huku na huku hakuweza kuwa nayo”
“Ikabidi asubuhi alipotoka hotelini akaenda kuniletea picha za mwanangu nione. Sasa wakati anakuja akaja amechelewa kwasababu mimi ndege yangu ilikuwa imeshakaribia ikabidi mimi nikarudi nikaacha vitu vyake pale reception, kurudi nampigia simu nitumie kwenye email sasa suala likaishia hivyo, yaani kila nikimpigia hapokei”.
Hivyo kwa maelezo ya Diamond hadi leo hajawahi kumuona mtoto huyo.




Leave your comment