EXCLUSIVE (TANZANIA) – Mimi sihusiki kabisa na madawa ya kulevya – Jux

 

Msanii Juma Jux akanusha madai ya kuuza madawa ya kulevya, baada ya aliyekuwa mpenzi wake Jackie Cliff kukamatwa na madawa ya kulevya nchini China na kufungwa, ni vitu vilivyomkosesha raha Jux.

Msanii huyo ambaye kwa sasa yupo nchini China kimasomo, amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa mikasa hiyo ilitikisa familia yake.

“Kitu kikubwa ni girlfriend wangu Jackie alipata matatizo na mpaka sasa kafungwa”, alisema Jux.

“Hii issue sawa ilikua inanihusu mimi kwa upande mwingine kutokana ni mtu wangu wa karibu na watu walikuwa wanajua lakini sasa kama ningekuwa sijulikani yote yasingeongelewa kwasababu kuna vitu vilikuwa vinaongelewa ambavyo vilikua vinaniaffect mimi na wazazi wangu”, aliongeza.

“Watu wengine walisema mimi nauza madawa ya kulevya wakati mimi sihusiki navyo kabisa. Lakini kama ningekuwa sijulikani na sio Jux, kila mtu ananijua na ndio maana ikatokea hivyo lakini ni kitu kilichoniumiza sana kwenye moyo wangu”.

Kwa hivi sasa msanii huyo ana mahusiano na msanii Vanessa Mdee.

Leave your comment

Top stories