EXCLUSIVE (TANZANIA) – Sina bifu wala ugomvi na Diamond – Mr Bue

Msanii wa Bongo Fleva Samir maarufu kama Mr Blue amesema kuwa hana ugomvi na Diamond baada ya kuibuka mzozo kwenye mitandao ya kijamii kuhusu nani mmiliki halali wa jina la ‘Simba’.

Blue ambaye kwa sasa anajipanga kuachia wimbo mpya akiwa na Ali Kiba mwezi huu, amekiambia kipindi cha The Weekend Chart Show cha Clouds TV kuwa aliamua kuweka wazi kwa umma juu ya umiliki wa jina hilo kama namna ya kusherehekea mafanikio baada ya wasanii kadhaa kumuiga.

“Kile kitu hakikuwa drama au ugomvi na mtu mimi nilifanya kama kujipongeza, kwasababu kama wewe ni shabiki yangu na unanifuatilia vizuri kipindi cha nyuma nilikuwa napost simba na slogan yangu “Simba kaamka na njaa kali” yaani baada ya kukaa muda mrefu bila ngoma nilivyokuja na kutoa ‘Pesa’ nikaandika ‘Simba kaamka na njaa kali’. Alisema.

Aliongeza “Pia nilitumia jina simba kutokana na kuwa na sauti ya kukwaruza kwenye muziki wangu. Sasa siku zilivyokwenda nikaona baadhi ya wasanii wengi tu, sio Diamond pekee wengine wapo Mwananyamala huko, Kigogo wanatumia jina la Simba. Ikanipa moyo kwamba kitu ambacho nimekigundua watu wamekikubali”.

“Kwahiyo nikapost kitu kwa kujipongeza, kwa kitu nilichokigundua miaka 2/3 nyuma leo kila mtu anataka kutumia. Lakini sasa mashabiki wanaichukulia vibaya kwasababu ana mashabiki wengi, angechukua mtu ambaye yupo chini yangu nadhani yasingetokea haya, kwahiyo naomba ieleweke sina ugomvi na Diamond na sijawahi kuwa na ugomvi na Diamond.

Leave your comment