EXCLUSIVE (TANZANIA) – Alichokisema AliKiba kuhusu Davido hiki hapa!

 

Mwaka 2015 staa wa Nigeria, Davido alitangaza kuwa mashabiki wajiandae kupokea collabo yake na Ali Kiba, kitu kilichowafurahisha mashabiki wengi wa muziki hususani wa Team AliKiba.  

I have a song coming out with AliKiba too, that’s gona be crazy” alisema Davido alipohojiwa na Millard Ayo kwenye Red Carpet ya tuzo za MTV MAMA mwaka jana 2015.

Kwa bahati mbaya hadi sasa tumeingia mwaka 2016 collabo hiyo haijafanyika wala  haina dalili ya kurekodiwa karibuni.

AliKiba amezungumzia mambo kadhaa kuhusu yeye na Davido pamoja na mpango wa collabo hiyo. Haya ni mambo matano aliyoyasema kupitia Ayo TV.

  • Ali Kiba na Davido hawajawahi kuwasiliana, lakini amewahi kuwasiliana na uongozi wa Ali Kiba.
  • Davido sio mshkaji wa Ali Kiba.
  • Davido ndiye aliyetamani kufanya collabo na Ali Kiba.
  • Hapo kabla Davido na Alikiba hawakuwahi kuongea chochote kuhusu kufanya collabo.
  • Davido anataka yeye na Alikiba wakae chini wafanye kitu kizuri.

Leave your comment