EXCLUSIVE (TANZANIA) – Millioni 40 zamgharimu Q Chief hadi kukamilisha bendi yake ya “QS International Band”

 

Msanii Q Chief amekamilisha maandalizi ya bendi yake mpya ya muziki iitwayo “QS International Band” anayodai imemgharimu zaidi ya  millioni 40.

Muimbaji huyo aliyeachia wimbo hivi karibuni ‘Mkungu wa Ndizi’ akiwa na TID, amesema huo ndio utakuwa mwisho wake wa kufanya show kwa kutumia play back.

“Sitofanya show yangu yoyote bila bendi yangu”, alisema. “Hii itanitoa kwenye daraja la kawaida kwenda lingine kubwa kwasababu kila muziki umebadilika kila msanii anataka kuwa na bendi. Sasa mimi kupewa hivi vyombo vilivyogharimu zaidi ya milioni 40 ni kama nimepewa almasi mkononi natakiwa kuitumia vizuri kwasababu tayari nimetoka kwenye misukosuko mingi ya maisha lakini siku zote nilikuwa na ndoto ya kumiliki vyombo na sasa hivi nimepata”, aliongeza Q Chief.

“Kwahiyo sasa hivi napenda kuwaambia mashabiki wangu huu ndio wakati wangu wa kufanya muziki ambao utawastaajabisha wengi” alisema Q Chief.

Na kuongeza kuwa sasa hivi yupo katika maandalizi ya kuwanoa vijana wa bendi hiyo huku akidai hataki kumweka mkongwe yoyote kwa kuhofia ujuaji.

Source: Bongo 5

Leave your comment

Top stories