EXCLUSIVE (TANZANIA) – Alichokisema Diamond kuhusu kukatwa jina la Nahreel ndani ya beat la‘Nana’ hiki hapa!
30 December 2015

Wiki chache zilizopita mtayarishaji wa muziki wa studio ya The Industry, Nahreel alilalamikia kuhusu kitendo cha utambulisho wake wa “Nahreel on the beat” kuondolewa kwenye wimbo wa ‘Nana’ wa Diamond ambaye yeye ndiye aliyeiproduce.
Ambapo kwa upande wa pili Diamond amepata nafasi ya kueleza sababu ya utambulisho huo kutokuwepo kwenye wimbo huo.
Platnumz amesema kuwa mwanzoni wakati anataka kushoot video hiyo Nahreel alimpa demo ambayo ilikuwa bado haijawekwa sign hiyo, hivyo baada ya kushoot na director kumaliza kuedit, alipopewa audio ambayo imekamilika ikawa imeongezwa sign, kitu ambacho kwa director ingempa kazi kutokana na kuongezeka kwa sekunde hizo ambayo kwenye demo iliyotumika mwanzo haikuwepo.

“So mara ya pili alivyonipa sasa video ilishaisha, nimepata iliyokuwa mastered ndio alikuwa ameweka sign” alisema Diamond kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM. “Haikuweza kufit kwasababu ilikuwa inazidisha sekunde halafu ilikuwa inaanza mwanzo mara kumi ingekuwa mwisho… inamaana editor aanze kukatakata na kuedit tena upya kitu ambacho tulikuwa tumeshachelewa. Kwahiyo ilichelewa kuwekwa ingekuwa imewekwa kuanzia mwanzo ingekua rahisi lakini sina sababu ya kusema nimkate producer kwasababu kama producer kafanya kazi yake kubwa lazima apewe credit zake” alisema Baba Tiffah.
“Ile nyimbo imefanyiwa mastering na Tudd Thomas, mtu anaweza kusema labda Tudd Thomas ndo kaichekecha, sio kweli na sioni sababu ya kumfanyia Mtanzania mwenzangu kutokumpa credit zake katika nyimbo aliyoitengeneza kutumia jasho lake nitakuwa na roho mbaya sana, Director aksema nataka iwe kama ilivyokuwa mwanzo mkinipa nyingine haiwezi kufit, aah sasa nitafanayaje kitaalam sijui mimi sijui mimi nikaona basi tukachukua ile ile ya mwanzo”, alimaliza Diamond.
Itazame video hiyo hapa;




Leave your comment