EXCLUSIVE (TANZANIA) – Ngoma mpya ya Temba yachelewa kutoka, Jua ni sababu gani na nani kasababisha!

 

Msanii Temba amedai kuwa Hanscana ndiye amesababisha kuharibika kwa ratiba yake ya kuachia video ya wimbo wake mpya, Fundi.

Rapper huyo ambaye miezi michache iliyopita aliwaahidi mashabiki wake kuachia wimbo wa ‘Fundi’ aliowashirikisha Yamoto Band na Jokate, na kusema kuwa kazi hiyo haitoweza tena kutoka mwaka huu.

“Nimeshindwa kutoa ngoma kwasababu nilipanga kutoa audio na video lakini director Hanscana akawa amesafiri South Africa kwa short project, lakini akakaa mwezi mmoja na nusu ndio maana nikashindwa kutoa project kwa nilihitaji kutoa video na audio” alisema Temba.

Pia Rapper huyo ametoa sababu nyingine ni kuingiliana na ratiba kati yake na Chege. Ambapo wasanii wote hao wapo chini ya management moja ya Mkubwa Fella.

“Kitu kingine wakati Chege anaenda Afrika Kusini na mimi nilitakiwa kwenda lakini nilishindwa kutokana na passport yangu iliisha muda. So nikaona bora nisupport kazi ya Chege halafu mwakani yakwangu ndio itoke”.

Source: Bongo5

 

Leave your comment

Top stories