EXCLUSIVE (TANZANIA) – Diamond aongelea suala la kutohudhuria Zari All White Party na si kumuogopa Ivan!
22 December 2015

Msanii Diamond Platnumz alikuwa Kampala, Uganda lakini pia hakuweza kuhudhuria party ya Baby mama wa mtoto wake Tiffah, Zari All White Party. Mpenzi wa zamani wa Zari, Ivan Ssemwanga na wapambe wake walihudhuria. Watu walihisi Diamond alihofia kwenda kumpa kampani mpenzi wake ili kuepusha shari ya Rich Gang ya Ivan.
Diamond amedai hakukacha party hiyo bali makubaliano aliyokuwa nayo na promota wa show yake siku ya Ijumaa (siku moja baada ya Zari All White Party) yalimtaka asiende kwenye party hiyo ili kutengeneza upekee wa kwenye show yake na Patoranking na iyo ukweli alikuwa akimgwaya Ivan.
“Halafu sasa watu wanasema namuogopa Ivan, mimi siwezi kumuogopa, hii code chafu kabisa kutoka Tandale mimi nimuogope mtu!”, alisema Diamond jana kwenye mahojiano katika kipindi cha Leo Tena cha Cloud FM.
Pia Diamond aliongeza kuwa ameshawahi kukutana na Ivan mara kibao japokuwa walipigiana mikausho kama kawa.
“Sijawahi kuwa na matatizo naye, nshakutana naye wakati naenda kwenye MTV alikuwepo, mara nyingi tulikuwa tunapishana hivi na hivi kabisa. Hatujawahi kusalimiana na kwasababu hatujawahi kuwa na mahusiano naye niseme nimsalimie ni uongo. Halafu nilikuwa nikipita nipo na crew, security yeye anakua tu anapita maskini ya Mungu” alieleza Diamond.




Leave your comment