EXCLUSIVE (TANZANIA) – Kuweza kutoka ubunifu unahitajika kwa muziki wa sasa– Cyril

 

 

Rapper Cyril Kamikaze, amesema muziki wa sasa sio tu kufanya video na ngoma kali ili uweze kutoka bali unahitaji kutumia ubunifu zaidi kukidhi viwango vyenye ubora na kufikia soko la kimataifa.

Mwanamuziki huyo amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kuwa watu wengi wanafikiri ukiwa na video nzuri ndio unafanikiwa.

“Unaweza ukawa na video kali halafu usihit, muziki ni zaidi ya chupa kali, ukirudishwa miaka fulani nyuma ngoma kali ndio ilikuwa inahit, lakini sasa msanii kupigwa na redio atataka kitu fulani. Hivyo muziki ni zaidi ya ngoma kali, zaidi ya chupa kali”, alisema Kamikaze.

Msanii huyo ameachia wimbo pamoja na video yake siku chache zilizopita ‘Shori’, pia amesema tayari ana album mbili ambazo zitatoka mwakani bila kujali kama zitamlipa au la.

Leave your comment

Top stories