EXCLUSIVE (TANZANIA) – Wimbo mpya wa Chege akiwa na Runtown (Nigeria) kutambulishwa leo MTV Base!
17 December 2015

Ni muda umepita tangu msanii wa TMK, Chege Chigunda alipoanza kuzungumzia swala lake la kufanya kolabo na msanii wa Nigeria, Runtown na Uhuru wa Afrika Kusini – Sweety Sweety. Hatimaye video hiyo iliyofanyika Afrika Kusini hivi karibuni itatambulishwa kwa mara ya kwanza kupitia MTV Base.
Video hiyo iliyoongozwa na Justin Campos wa Gorilla Films itaonyeshwa kwenye Spanking New ya MTV Base, Alhamisi ya leo hii Dec 17, saa 12 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Video hii inamfanya Chege kuongezeka katika list ya wasanii wa bongo waliofanya collabo na wasanii wa Nigeria kama Vanessa Mdee, Diamond na Shetta.




Leave your comment