EXCLUSIVE (TANZANIA) – Chekecha ni kama dhahabu kwangu – Ali Kiba

 

 

Msanii wa Bongo Fleva anayefanya vizuri katika soko la muziki Tanzania na Afrika amedai nyimbo yake ya ‘Chekecha Cheketua’, ndio wimbo uliopokelewa vizuri kuliko nyimbo zake zote alizowahi kutoa.

Msanii huyo ambaye pia ni balozi wa Shirika la Kimataifa la WildAid, ameiambia BBC kuwa wimbo huo uliweza kuhit ndani ya siku moja.

“Nyimbo yangu ya ‘Chekecha’ jinsi ilivyopokelewa haijawahi kutokea katika maisha yangu ya kimuziki toka naanza. Chekecha kiukweli ilichukua siku moja kuhit” alisema.

Katika mahojiano hayo pia Kiba aliulizwa kuhusu mpango wake wa kujitanua zaidi kimataifa kama wasanii wengine wa Tanzania walivyofanya. “Nataka nifike kidunia zaidi kwasababu I have been there na nilivyorudi hata kama watu walisahau nimeshawakumbusha”.

Leave your comment

Top stories