EXCLUSIVE (TANZANIA) – FA atoa Sababu ya kutengeneza video mbili za ‘Asanteni kwa Kuja’
16 December 2015

Baada ya Mwana FA kuachia wimbo mpya wa ‘Asanteni kwa Kuja’ wiki hii, amesema kuwa video ya wimbo ulioshutiwa Afrika Kusini ina version mbili (Dirty & Clean), safi ikiwa ni kwaajili ya TV za nyumbani na chafu kwaajili ya TV za nje.
Akizungumza na kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, FA amesema maamuzi ya kufanya version mbili yalikuja baada ya kuwa na mabishano kati yake na director wa video hiyo kuhusu kipi kitoke na kipi kibaki.
Amesema baada ya kutumiwa video aliona kuna vipengele vingi ambavyo visingefaa kuonyeshwa kwenye runinga za hapa nyumbani, hivyo alitaka sehemu hizo ziondolewe huku director wake akikataa kuziondoa.
“Video ilivyokuja nikamwambia hii video ilivyo local channel za hapa kwetu haiwezi kuonyeshwa, ikabidi nimwambie sekunde hii mapaka hii inabidi utoe, jamaa akabisha kabisa akasema hiyo ndiyo video yenyewe, kwahiyo atachoweza kufanya ni kuziondoa zile parts ambazo nimesema, lakini huku ambako ana uhakika video inacheza jinsi ilivyo ataipeleka kama ilivyo, haikuwa lengo langu kutengeneza video mbili ila mazingira yalinipeleka huko”, alisema Mwana FA.
Mwana FA aliongeza kuwa hakufahamu moja kwa moja kama director alipanga kufanya video ya namna ile.
“Mi nililetewa script lakini haikuwa na details moja kwa moja kwamba watu watakuwa wamevaa nini, wata act vipi, mi mwenyewe ilibidi nisafiri na begi mbili kuhakikisha nina kila kitu ninachokitaka, ulipofika muda ndo nikaona wamevaa hivi, wanakuwa directed wafanye hivi”, alisema FA.




Leave your comment