EXCLUSIVE (TANZANIA) – Una single moja halafu unatafuta meneja hiyo ni dalili ya uvivu – AY
15 December 2015

Mzee wa komesho Ambwene Yesaya maarufu kama AY, amewataka wasanii wachanga kuacha kutafuta watu wa kusimamia kazi muziki wao, bali watengeneze kwanza connection zao wenyewe.
Mwanamuziki huyo anayemiliki kampuni ya Unity Entertainment ya kusimamia wasanii amekiambia kipindi cha Mkasi cha EATV, kuwa anashangaa kuona msanii ana ‘single’ moja lakini anatafuta meneja wakati alitakiwa kujijenga mwenyewe.
“Sasa hivi mtu hana hata single au ana single moja, hajapata experience ya kutengeneza hit song nne ili kujipima yeye na wasanii waliopo kwenye game hapo hapo anataka meneja, wakati biashara ni yake”, alisema. “Huwezi kuwa na meneja wakati wewe mwenyewe hujaijua biashara yako hata kwa kiasi fulani. Kwahiyo nimeshaiona na nimeshaongea na wasanii hiyo ni dalili ya uvivui” aliongeza AY.
“Ndio maana nikasema mwanzo wa muziki kwa watu ambao wanaanza sasa hivi kwanza ni lazima ujue watu. Kama wewe ukiwa na meneja unakaa nyumbani hao watangazaji utawajuaje? Lazima utengeneze wewe mwenyewe binafsi ili ujuane na watu. Baada ya hapo wewe ndio mwenye brand, meneja anakuja anakukuta upo vizuri”.




Leave your comment