EXCLUSIVE (TANZANIA) – Ujio wa “Christian Bella House of Talents” yakwake Bella

 

Msanii wa muziki Christian Bella ameweka wazi mpango wake wa kuanzisha lebo yake ya muziki ya ‘Christian Bella House of Talents’ itakayosaidia vijana wenye vipaji vya kuimba.

Mwanamuziki huyo aliyeachia wimbo ‘Acha Kabisa’ akiwa na Koffi Olomide hivi karibuni, ambapo ameiambia tovuti ya Bongo 5 kuwa amefanya hivyo ili kuwasaidia vijana wanaohitaji msaada wake.

“Mpango wangu mkubwa kwa mwaka 2016 ni kuanzisha record label yangu ambayo itaitwa Christian Bella House of Talents”, alisema.

“Itakuwa inasaidia vijana wenye vipaji. Vijana wengi wanakuja kwangu kutaka msaada na njia ya kuwasaidia ni kuanziasha label. Tayari imefikia pazuri mpaka sasa, nimeshaanza kutengeneza studio na soon itakamilika. Hiyo itakuwa mwakani nitaanza kutafuta wale vijana wenye vipaji vya ukweli na kuanza kuwasimamia kabisa. Yaani nitaingia nao studio kurekodi kushoot video pamoja na interview”, aliongeza.

Pia amedai kuwa atakuwa anatoa mafunzo ya vocal na pamoja na matumizi ya vifaa ili kuweka vizuri zaidi ili kukabiliana na changamoto la soko la muziki. Katika hatua nyingine Bella amesema yupo kwenye maandalizi ya kwenda kushoot video ya wimbo wake ‘Acha Kabisa’ nchini Dubai akiwa na Koffi Olomide.

Leave your comment

Top stories