EXCLUSIVE (TANZANIA) – Unapopata pesa huna budi kuwekeza kwenye muziki wako – Maste J

 

 

Mtayarishaji wa muda mrefu wa muziki na mwazilishi wa MJ Records, Master J, amesema muziki wa Tanzania ulipofika ni wakati wasanii kujitambua na kwendana na wakati kuanzia kazi zao hadi muonekano kwa watu.

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio wiki iliyopita, Master J alisema ni vizuri msanii awe na timu itakayomsaidia kuboresha muziki wake.

“Unajua kama msaniii ukishafika level fulani kwenye jamii au soko lolote, kwenye macho ya watu umekuwa kama brand tuseme, unavyokuwa kwenye video unaonekana kama star, kwahiyo ni lazima uwe na timu mahususi ambayo ndiyo inakushauri”, alisema.

Pia Master J aliongeza, “ Lakini mimi ninaona tutafika kwasababu soko letu lilikuwa dogo na hela ilikuwa ndogo, sasa hivi wasanii wanatengeneza hela nyingi, the more money they have inamaanisha wanaweza wakawa na timu, kuna wengine wameshakuwa na timu. ana management, ana DJ ana Stylist”.

Leave your comment

Top stories