EXCLUSIVE (TANZANIA) – Unajua nani ameandika ‘One More Night’ ya Jux? Mtambue ni nani!
14 December 2015

Msanii wa Bongo Fleva Juma- Jux wiki iliyopita ameachia video na audio ya wimbo wake mpya uitwao ‘One More Night’. Msanii huyo ameeleza kuwa Walter Chilambo ndiye aliyemwandikia wimbo huo na jinsi ilivyokuwa hadi kumuandikia wimbo huo.
“Mimi nimekutana tu na msichana ninayemuimbia mara moja tu. Sasa baada ya hapo msichana hakutaka tena uhusiano na mimi, lakini mimi natamani tuendelee au itokee One More Night kama ile ya mwanzo” alisema Jux.
Jux akiongea na Millardayo.com “ Walter ameandika wimbo huu na mimi nilikuwa nataka kufanya kitu cha tofauti kabisa, kama kawaida tumekuta beat na Walter alikua na idea ya kuandika wimbo wa aina hii. Kwasababu nimeandika sana nyimbo mimi mwenyewe, sasa hivi nilitaka kujaribu kitu cha tofauti, so kuanzia uandishi hadi melody ni kazi ya Walter Chilambo”,
Tazama video hiyo hapa chini;




Leave your comment