EXCLUSIVE (TANZANIA) – Diamond Platnumz kufanya tour Ulaya 2016, Cheki ratiba yake hapa!
11 December 2015

Msanii wa Bongo Fleva na mshindi wa tuzo mbalimbali Diamond Platnumz anatarajia kufanya tour barani la Ulaya, 2016. Mbali na kuwa na ushawishi mkubwa pia amekuwa akiripotiwa kuwa kati ya wanamuziki wanaouza sana kwa Afrika Mashariki kwa sasa.
Tuzo za BET 2014 zilimtambua kama msanii maarufu wa Bongo Fleva toka Tanzania. Hitmaker huyo wa “Number One” uliomfanya kuchaguliwa kuwa nominated katika kipengele cha ‘Best International Act’: Africa katika BET Awards.
Wakati mashabiki wakisubiri wimbo wake mpya, msanii huyo ameibuka na kushare na mashabiki tour atakayoifanya huko nchi za Ulaya 2016. Tour hiyo itakayoanza mwezi March 19, ambapo atatembelea nchi 7 ikiwemo Denmark, Ufaransa, Norway, Finland, Sweden na Ujerumani.
Mwaka 2016 tayari umeonekana kuwa mwaka wenye mambo mengi kwa msanii huyo, hivi karibuni alishinda tuzo za AFRIMA katika kipengele cha “ Artiste of The Year and Song of The Year’.
Hapa Chini ni ratiba ya Tour hiyo;





Leave your comment