NEW SONG (TANZANIA) – Diamond Platnumz kuachia wimbo mpya Ijumaa hii
10 December 2015

Diamond Platnumz kuachia wimbo mpya hivi karibuni unaoitwa ‘Utaipenda’. Msanii huyo anayetamba na kibao cha ‘Nana’ aliomshirikisha Mr Flavour.
‘Utaipenda’ ni wimbo ambao mashabiki wamekaa kuusubiria kwa muda mrefu na hatimaye kesho ijumaa msanii huyo ameahidi kuachia wimbo huo. Imebainika kwamba sababu mojawapo ya kuchelewesha wimbo huo imetokana na Daktari bingwa wa magonjwa ya Uzazi Dr Mwaka, Tanzania aliyemwagia mamilioni ya pesa kwa ajili ya kuitangaza kliniki yake iliyopo Ilala Bungoni.
Taarifa hizo zinasema kuwa hiyo ndio sababu kubwa iliyomfanya kusogeza mbele utoaji wa wimbo huo hadi Ijumaa baada ya kupata ofa hiyo. Ambapo inasemekana kiasi alichopata ni kama Mil 50 za kitanzania toka kwa daktari huyo.
Ambapo katika post zake za Instagram anaweka hashtag ya #DrMwaka. Hapo ndipo ule usemi wa waswahili ‘Mwenye nacho huongezewa zaidi’.




Leave your comment