04- EXCLUSIVE (TANZANIA) – Tutawalipa Wasanii kwa nyimbo zao kupigwa kwenye TV na Radio- Ruge

 

 

 

Mdau mkubwa wa muziki hapa nchini na Mkurugenzi na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amesema ujio wa kampuni ya kusimamia hakimiliki za wasanii, Copyrights Management East Africa Limited (CMEA) wakishirikiana na Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA), utasaidia vituo vya redio na runinga kushindwa kukwepa mirahaba unaotokana na upigwaji wa nyimbo za wasanii.

Akizungumza na CMEA hivi karibuni, Ruge alisema mfumo huo mpya utawasaidia wasanii kunufaika na kazi zao.

“Ni jambo ambalo litawakilisha kazi za wasanii katika kuweza kulipwa pale ambapo nyimbo zao zitakapokuwa zinapigwa redioni. Vyombo vya habari haviwezi kukataa kwasababu ukubwa wetu, umaarufu wetu na tuna ubia wa kibiashara kati ya maudhui tunayopata na kutokana na kazi za sanaa na maudhui mengine tunayatengeneza sisi wenyewe. Kwavyovyote vile ili kukua na kujivunia, hapa vyombo vyetu vya habari lazima tujivunie ukarimu uliotokea kati yetu na CMEA na COSOTA”, alisema Ruge.

Pia amesema katika hatua nyingine Ruge amesema mfumo huo utawanufaisha zaidi wale wanaofanya muziki mzuri.

“ Matokeo makubwa yatakayotokea kwenye Sanaa yetu wapo watakaofanikiwa na wapo ambao hawatafanikiwa. Hii ni kama biashara zingine unazoziona, wale wanaofanya vizuri watafanya vizuri na wale wasiofanya vizuri wasikate tamaa, waboreshe kazi zao ili wafanye vizuri” aliongeza Ruge.

 

Leave your comment

Top stories