EXCLUSIVE (TANZANIA) – Tamasha la Fiesta halitokuwepo mwaka huu – Ruge

 

 

Baada ya staa wa Nigeria kuahidi mashabiki kuwa angerudi tena Tanzania katika tamasha la Fiesta Disemba mwaka huu, lakini taarifa mpya ya kutoka kwa waandaaji wa Clouds Media  zinasema tamasha hilo halitakuwepo mwaka huu.

Mkurugenzi wa uzalishaji wa vipindi Clouds Media Group, Ruge Mutahaba ametoa sababu za kutofanyika kwa tamasha hilo kubwa mwaka huu.

“Fiesta mwaka huu tumekubaliana tusiifanye kwasababu tutakuwa tunabanana”, amesema Ruge kupitia XXL ya Clouds Fm. “Tulijua tukimaliza kampeni tutafanya kwamikoa michache lakini tumeona kwamba hakuna kitu kizuri kama kumsupport mheshimiwa Magufuli, hebu sasa hivi turudi kwanza tutulie tuache hii amsha amsha aliyoanza nayo ianze kufanya kazi tujipange kwaajili ya Fiesta 2015 ambayo itafanyika mwaka kesho, tutakuwa tunafikisha miaka 15 ya Fiesta na nina uhakika itakuwa na ukubwa inayostahili kufanya kitu kidogo mwaka huu tumeona tuache mwaka kesho mikoa 15 ya miaka 15 ya Fiesta itakuwa kubwa zaidi. Hapa Kazi imebidi iivae Fiesta pia” asema Ruge.

Leave your comment