EXCLUSIVE (TANZANIA) – Mastaa wapo kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi (TACAIDS)
2 December 2015

Dunia imeadhimisha siku ya Ukimwi duniani jana Disemba 1, Tume ya kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) imesema watu maarufu wakiwemo wasanii wana hatari zaidi ya kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutokana na ushawishi wao na hivyo wanatakiwa kupewa elimu.
Mwenyekiti wa TACAIDS, Dr. Fatma Mrisho akizungumza na Global Shapers Community Dar es salaam, alisema ushawishi wa wasanii hao unawafanya watamaniwe na watu wengi hali inayowaweka kwenye hatari.
"Watu wa muziki na burudani ni watu wenye ushawishi mkubwa sana", alisema. "Wao wenyewe wapate elimu ili wajikinge kwanza halafu ujumbe kwasababu wanafuatwa sana. Ni watu ambao wana mvuto sio tu kwa vijana hata mimi ni watu ambao nawapenda sana kwenye muziki kwahiyo ningependa kuwasikia na wazungumze masuala ya Ukimwi", alisisitiz Dr Fatma.
Pia aliongeza kuwa anavutiwa na utunzi na juhudi za wasanii mbalimbali wakiwemo Diamond Platnumz, Alikiba na Lady Jay Dee.
Tazama video hapa;
<iframe width="560" height="315" src="https://www.youtube.com/embed/Lv6gPbZkIIE" frameborder="0" allowfullscreen></iframe>




Leave your comment