Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
EXCLUSIVE (TANZANIA) – Shaa kukerwa na tabia ya mashabiki kumpambanisha na Vanessa mdee
2 December 2015

Mwanadada Sarah Kaisi aka Shaa ameeleza ni kwa jinsi gani huwa anakerwa na baadhi ya mashabiki wanaojaribu kuwashindanisha kisanii na muimbaji mwenzake Vanessa Mdee.
Muimbaji huyo wa ‘Sugua Gaga’ ambaye wiki iliyopita ametoa wimbo mpya unaitwa ‘Toba’, amesema sio sawa kushindanishwa na Vee Money kwasababu wote wanaiwakilisha bendera ya Tanzania.
“Niwaambie ukweli sipendi sana hii tabia ya watanzania kunishindanisha na Vanessa Mdee au kitendo cha kuwashindanisha wasanii wa nyumbani”, alisema Shaa kupitia Planet Bongo ya EATV. “Huwezi kuwashindanisha watu ambao wapo kwenye boti moja, Mimi Shaa pamoja na Vanessa Mdee wote tunapeperusha bendera moja ya Tanzania hivyo unapotupambanisha ili iwe nini? Ni bora hata ungenipambanisha na msanii kama Yemi Alade sababu yule ni msanii kutoka nchi nyingine” aliongeza Shaa.
Weekly Top 10 songs
Top stories
- Jalingo
04 May
- Redice1 story
04 May
- Parsonal background
04 May




Leave your comment