EXCLUSIVE (TANZANIA)- Mimi na Aika tulianza kuishi pamoja tukiwa na godoro tu- Nahreel

 

Mtayarishaji na muimbaji wa muziki anayeunda kundi la Navy Kenzo pamoja na mpenzi wake Aika, amesimulia maisha ya yeye na mpenzi wake. Kabla ya kuanzisha kundi lao, wawili hao walikua wanaunda kundi la Pah One pamoja na wasanii wengine.

“Mimi na Aika tumekutana tukiwa masomoni India, wote tulikuwa tunasomeshwa na wazazi wetu, tumepitia mambo mengi sana tukamaliza shule tukaja Tanzania” Nahreel alikiambia kipindi cha Mkasi cha EATV.

“Mimi nikawa nimeajiriwa na Aika akawa ameajiriwa lakini  baadaye tukaona muziki wetu unapotea, kwasababu tumeingia kwenye kazi nyingine. Kwahiyo tukaamua kuja Dar ili kufanya mambo ya muziki”, aliongeza.

“Kwahiyo tulianza chini sana, tulianza with nothing, nilikuwa na godoro dogo ambalo nilianza na Aika. Tulikuwa tunalala kwenye hilo godoro mimi na Aika. Tukaanza hivyo huku tunafanya muziki. Mimi nafanya production zangu na Aika anafanya shughuli zake za mitindo, ndio hivyo tumetokea kwenye vitu vingi tukajenga mpaka hapa tulipofika”

“Tumepambana sana mpaka kufika hapa” alimalizia Nahreel. 

Leave your comment