EXCLUSIVE (TANZANIA)- Nasibu Abdul angekuwa mume wangu wa maisha –Wema Sepetu

 

Miss Tanzania 2006 na muigizaji wa filamu Wema Sepetu bado anamkumbuka Nasibu aliyewahi kuwa mpenzi wake. Nasibu Abdul ambaye ni maarufu kwa jina Diamond Platnumz.

Wema Sepetu alikuwa akijibu swali kwenye kipindi cha Hitzone kupitia kipindi cha redio cha Jembe FM cha Mwanza, alipoulizwa ni mwanaume gani ambaye alitamani awe mume wake wa ndoa.

“Ni yupi ambaye niliwahi kusema huyu anaweza kuwa wa maisha, alisema Wema ‘Kiukweli alikuwa anaitwa Nassib Abdul, nilishawahi kusema hivyo” alisisitiza.

Lakini ndoto hiyo iliyeyuka baada ya wapenzi hao kuachana mwaka jana na Diamond kuhamisha mapenzi yake kwa Zarina Hassan (Zari the Bosslady) ambaye tayari wana mtoto wa kike pamoja “Latifah”.

Leave your comment