Mapinduzi Ya Wanawake Kwenye Muziki.

[Image:Mdundo.com]

Writer:Elizabeth Betha

Download Ohangla Dj Mixes on Mdundo.com

Mwezi huu wa tatu (3) tumeendelea kusherekea wanawake duniani, kupitia hapa Mdundo tovuti bora ya muziki Afrika wanawake wanaofanya shughuli za muziki wameweza kupata maua yao kwa ukubwa. Ni wazi kuwa wanawake kwenye tasnia ya muziki Tanzania wameonesha mageuzi makubwa ya kimuziki ukilinganisha kwa miaka ya nyuma, ambapo wanaume walitawala zaidi soko la muziki.

Muziki wa Bongofleva umezalisha vipaji vingi sana vya wanawake wenye vipawa vya hali ya juu, na ni wazi kwa miaka ya hivi karibuni wanawake katika muziki wamezidi kupenya katika soko la muziki la kimataifa. Kwa miaka ya nyuma hari ilikuwa kwa kasi ndogo na kollabo nyingi za kimataifa zilifanywa na wanamuziki wa kiume na wachache wa kike kama kina Lady Jaydee, Ray C na wengine.

Kwasasa si tu kollabo za kimataifa ila hata matamasha makubwa ya muziki, utaarishaji wa muziki, maDJ wa muziki ni wanawake, hii inaonesha kuwa wanawake wameweza kupiga hatua kubwa sana kwenye tasnia ya  muziki hapa Tanzania.

Msanii Nandy alianza safari yake ya muziki na baadae ya kushiriki mashindano ya uimbaji ya Tecno Own the Stage mwaka 2016 na kushika nafasi ya pili. Kutoka hapo ameweza kutoa nyimbo nyingi nzuri zilizokonga mashabiki zake na wadau wa muziki ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Pamoja na uimbaji na uandishi wa muziki, ameweza kuandaa tamasha la muziki alilolipa jina la Nandy Festival ambalo alilianzisha mwaka 2019. Kupitia tamasha hilo ameweza kuwapa nafasi zaidi wasanii wa kike kung’aa, tamasha limeweza kuwa endelevu na limefanikiwa kuwafikia mashabiki wa muziki katika mikoa mingi ya Tanzania.

Pamoja na hayo, Nandy pia ni mmiliki wa lebo ya muziki aliyoipa jina la The African Princess Label, mpaka sasa anasimamia kazi za msanii Yammi ambaye ni mwanadada mwenye kipaji na sauti ya kuvutia sana, Yammi pamoja na Nandy wana kollabo yao kali inayoitwa Lonely, ni wimbo unaofanya vizuri sana toka walivyoutoa. Unaweza kuona kuwa Nandy si mwanamuziki tu bali pia ni mfanyabashara wa muziki kwakuwa na yeye anang’arisha vipaji vya wanawake wenzie kwa ukubwa sana.

Tumebarikiwa kuwa na Abby Chams, msanii wa kike mwenye vipaji vingi ukiachana na uimbaji. Abby Chams anaweza kupiga vyombo vya muziki kama piano, violin, guitar na vinginevyo. Ni wazi toka ameanza kufanya kazi za muziki haiwezi kupingwa kuwa ni msanii ambaye anajiweza, ameweza kutoa hits za kutosha na hivi karibuni kollabo yake na mkali Harmonize inayoitwa Me Too ambayo inafanya vizuri sana.

Abby ambaye ukiachana na kuimba, kuandika muziki, kupiga vyombo vya muziki anaweza pia kuandaa muziki yaani ni music producer anaechipukia, na  kwa hapa Tanzania ni kazi inayofanywa na wanaume zaidi. Ni wazi kuwa ataweza kuleta mageuzi mazuri kwenye tasnia ya muziki na kuwapa ujasiri zaidi wanawake wengine kufanya muziki kwa uhuru na kupata mafanikio.

Wasanii wa kike Tanzania wameonesha uwezo mkubwa wa kubeba soko la muziki kwa miaka ya karibuni, na inaonesha miaka inayokuja wataendelea kupanda chati zaidi kwakuwa wanafanya kazi nzuri sana na bado kuna nafasi ya wengine kuongezeka ili kuleta chachu zaidi kwenye kiwanda cha burudani Tanzania.

 

Leave your comment