Ujio Mpya Wa Goodluck Gozbert
29 January 2025
[Image Source: Instagram]
Writer: Elizabeth Betha
Download Kamba Dj Mixes On Mdundo
Tukianzia sasa au nyuma kumuhusu Goodluck, kote haitabadilisha kitu kimoja muhimu ambacho ni kuwa mwamba ana kipaji na ubunifu wa hali ya juu, na ndio maana hata leo bado anaendelea kuwako katika tasnia ya muziki kama mtu anaekubalika na mashabiki na hata wasanii wenzie ikiwemo wa muziki wa injili, Bongofleva, lakini pia wadau wa muziki.
Goodluck Gozbert ni msanii wa muziki wa injili na kwa yeye anapendelea kujulikana kama mtumishi wa Mungu na huduma yake ni uimbaji na utunzi wa nyimbo. Amekuwako kwenye kiwanda cha muziki kwa miaka mingi akifanya muziki wa injili tangia mwanzoni.
Alijizolea umaarufu kwa nyimbo kama Shukrani, Ipo Siku, Kama Si Wewe na nyingine nyingi ambazo kwa ujumla ziligusa maisha ya watu wengi na kumfanya Goodluck jkujizolea mashabiki wengi hususani wapenzi wa muziki wa injili ndani na nje ya Tanzania. Aliweza kufanya kazi pia na wasanii wa muziki wa Bongofleva kwa kuwafanyia utunzi wa nyimbo zao, na pia kushikikishwa na wasanii wa Bongofleva kwenye kazi zao ikiwemo Mama yake Ben Pol iliyotoka March 2020.
Kwenye tasnia ya muziki wa injili, huwezi kuacha kumtaja Goodluck Gozbert kama msanii mzuri na ukiongeza pia ni mmoja ya waanzilishi wa kizazi kipya wa muziki wa injili kwa hapa Tanzania, kwasababu muziki wa zamani na wa sasa wa injili ni tofauti na mageuzi hayo yamechangiwa sana na vijana waliojitokeza na kushika usukani kwa kuongeza ubunifu huku wakiendelea kumtumikia Mungu.
Hivi karibuni Goodluck Gozbert aliachia EP yake aliyoipa jina la Ushindi ikiwa na takribani nyimbo sita, mpaka sasa EP hiyo ina mwaka mmoja toka itoke, na aliweza pia kushirikishwa kwenye albamu ya Msanii Bora wa Hip Hop yake Stamina, akiwemo kwenye Nakuja ambayo ni moja ya kazi nzuri kwenye albamu hiyo.
Pamoja na yanayoendelea kwasasa kwake Goodluck, likiwemo tukio la kuchoma gari alilipewa na Nabii Geor Davie, haijamzuia kuendelea kufanya anachokipenda ambacho kuimba na sasa ameachia wimbo wake mpya kabisa alioupa jila la Wao Nyeshe ambao ni kama maombi yake kwa Mungu, ni wimbo mzuri ambao mtu yoyote anaweza kuimba na kuufurahia kwasababu una ujumbe mzuri.
Tuendelee kusapoti muziki wake kama ilivyokuwa hapo nyuma, ili huduma yake izidi kuwa kubwa na wapenzi wa muziki waendelee kubarikiwa na muziki wake. Share hapo kwenye comments muziki wako pendwa kutoka kwa Goodluck Gozbert.
Leave your comment