Kusherehekea Legend wa Tanzania: Prof. Jay na Mchango Wake Katika Muziki

[Image Source: Instagram]

Writer: Hoboka Asukile

Download Kamba Dj Mixes On Mdundo

Prof. Jay ni gwiji kwenye tasnia ya muziki Tanzania na pia ni miongoni mwa wasanii walileta mapinduzi ya kitofauti sana kwenye muziki wa Tanzania. Kuanzia mwaka 2000, amekuwa akitutuburudisha na pia kutuelimisha katika masuala tofauti ya kijamii. Professa Jay kabla ya kujikita katika maswala la kisiasa aliwezea kuachia nyimbo nyingi ambazo bado zina sikika na kupendwa na wengi nchini kama Zali la Mentali, Nikusaidiaje, Ndivyo sivyo, ndio mzee, Bongo Dar-es-salaam pamoja na zingine nyingi tu.

Si tu msanii, bali pia ni kiongozi wa mawazo! Kuingia kwake kwenye siasi kulionesha utayari na ari yake kubwa ya kutaka kubadilisha maisha ya wengi, kupelekea kukubalika sana na watanzania wengi pia aliweza kuonyesha wasanii wenzie kwamba muziki ni sanaa inayoweza kukupa heshima kwa watu.

Kusema ukweli tasnia ya Mziki wa Bongofleva na hip hop nchini imeipitia mabadiliko mengi kulingana na vitu vingi vinavyoendelea ila ni ukweli usiopindika kwamba mchango wa professa Jay bado unaonekana mpaka sasa kwani amekuwa mwalimu na mentor kwa wanamziki wengi wa kizazi kipya. Hivyo Professa kushtahili Maua na pongezi za dhati kwa mchango wake katika tasnia ya mziki Tanzania.

Wakati tunasherehekea michango yake, pakua DJ mixes za Prof. Jay. Utajikuta unacheka na kuimba, “Ndio Mzee” 

Leave your comment