EP Mpya ya Ali Kiba "Starter": Hatua Inayoashiria Ukubwa wa AlikIba Katika Muziki.

Mhariri: Hoboka Asukile.

Pakua Djmix mbali hapa

EP mpya ya Ali Kiba, Starter, inatarajiwa kuzinduliwa kwa kishindo tarehe 20 Septemba, 2024, na tayari imezua gumzo kubwa kwenye ulimwengu wa muziki. Hii ni hatua nyingine muhimu katika safari ya muziki wa Ali Kiba, ikidhihirisha uwezo wake wa kuchanganya mitindo tofauti ya muziki na kushirikiana na mastaa wakubwa wa Bongo Flava na Afrobeat.

Starter inajumuisha nyimbo kali kama "Nahodha," "Top Notch" (aliyomshirikisha Marioo), "Hatari" (ft. Jay Melody), na "Bailando" (ft. Nandy). Hii ni ishara ya ubunifu wa Ali Kiba na uwezo wake wa kufanya kazi na wasanii wenye vipaji, kama Nandy, Jay Melody, na Marioo. Kila wimbo umebeba ladha ya kipekee, ukiunganisha mtindo wa Kiba tunaoufahamu na miondoko ya kisasa zaidi.

EP hii inadhihirisha ukuaji wa Ali Kiba kama msanii na inaonyesha namna anavyoendelea kuvuta hisia za mashabiki wake kwa ushirikiano wa kuvutia na maudhui ya kibinafsi. Hakikisha haupitwi na uzinduzi huu na tembelea Mdundo.com ili upate DJ mix bora zinazobeba ladha ya Bongo Flava na Afrobeat!

Leave your comment