WCB Wasafi Kutambulisha Wasanii Wawili Mwaka Huu

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Miezi michache baada ya kumtambulisha D Voice msanii, Diamond Platnumz ametangaza kuwa yuko mbioni kutambulisha wasanii wengine wawili mwaka huu.

Mara ya mwisho kwa lebo ya WCB kutambulisha msanii mpya ilikuwa ni Novemba mwaka jana walipomtambulisha D Voice kama msanii rasmi wa lebo hiyo.

Tangu kutambulishwa kwake, D Voice ameachia EP moja ya kuitwa Swahili Kid yenye nyimbo 10.

Akizungumza wakati akiwa anatumbuiza kwenye jukwaa la Serengeti Bites Vibes, Diamond alisema kuwa WCB Wasafi wana mpango wa kutambulisha msanii mwingine mwaka huu na kwamba wasanii wote wenye vipaji wanakaribishwa kwenda kuonesha uwezo wao

Mwaka huu tunataka tutoe wasanii wengine wawili. Na kwa sasa hivi hatuna. Kama unajua kuimba usiogope njoo usafini" alizungumza Diamond akiwa jukwaani.

Ikumbukwe kuwa lebo ya WCB ilianza rasmi mwaka 2015 na msanii wa kwanza kutambulishwa alikuwa ni Harmonize.

Kufikia sasa lebo hiyo ina wasanii watano ambao ni Diamond Platnumz, Zuchu, Mbosso, Lava Lava, D Voice na Queen Darleen.

Wasanii ambao wameshawahi kuwa sehemu ya lebo hiyo ni pamoja na Harmonize aliyeondoka 2019, Rich Mavoko aliyeondoka mwaka 2018 pamoja na Rayvanny ambaye aliondoka mwaka 2022.

Leave your comment