"Sina Wimbo Ninaoupenda Kutoka Tanzania" Cassper Nyovest

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Msanii kutokea Afrika Kusini, Cassper Nyovest hivi karibuni amezua utata baina ya mashabiki baada ya kusema hakuna ngoma yoyote anayoipenda kutoka Bongo.

Cassper Nyovest ametoa kauli hiyo hivi karibuni baada ya kutua nchini Tanzania kwa ajili ya kutumbuiza kwenye tamasha la Serengeti Bites Vibes.

Akiwa anaongea na vyombo vya habari, Cassper Nyovest aliulizwa swali kuhusu ngoma aipendayo kutoka Tanzania na ndipo alidokeza kuwa hakuna ngoma yoyote kutoka Tanzania anayoipenda.

"I don't have one, I don't have one. I have to re-up" alizungumza Cassper Nyovest muda mchache baada ya kutua Tanzania.

Cassper Nyovest alikuja nchini Tanzania kwa ajili ya Serengeti Bites Vibes, tamasha ambalo pia wasanii wengine kama Diamond Platnumz, Jaivah, Billnass, Darassa, Chino Kidd, Abigail Chams na D Voice pia walikuwa wanatumbuiza

Leave your comment