Nandy Aachia Ngoma Mpya "Wahala"

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Msanii nguli kutokea nchini Tanzania, Nandy amerudi tena kwenye kiwanda cha muziki na ngoma mpya ya kuitwa "Wahala"

"Wahala" ni mradi wa nne kutoka kwa Nandy kwa mwaka huu baada ya mapema mwaka huu kuachia "Daah" na remix zake mbili.

Kwenye "Wahala" Nandy anapita kwenye muziki aina ya Amapiano ambayo imechanganywa na vionjo vya Bongo Fleva.

Humu ndani, Nandy anaonesha kuwa hayuko tayari tena kuumizwa kwenye mapenzi ambapo kwenye mashahiri ya wimbo huu, fundi huyo wa Bongo Fleva anamuomba mpenzi wake asimuumize tena kama ambavyo aliumizwa huko zamani.

"Wahala" imetayarishwa na Kimambo Beats, producer kutoka Tanzania ambaye pia alishiriki kuandaa ngoma nyingi za Nandy

Leave your comment