Ngoma Mpya: Jay Moe Na Country Wizzy Warudi Tena Na "Mocassin"

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Ushirikiano baina ya rapa Country Wizzy na Jay Moe umeendelea kuwa wa moto na hii ni baada ya wasanij hao kuachia ngoma mpya ya kuitwa "Mocassin"

Wawili hao wiki chache nyuma waliachia "Way Back" ngoma ambayo ilipokelewa vyema na mashabiki ndani na nje ya nchi.

Kwenye "Mocassin" Jay Moe na Country Wizzy wanaonesha uwezo wao mkubwa wa kurap ambao kwenye ngoma hii marapa hawa wanajisifia namna ambavyo wanajua kupendeza na kuvaa vizuri.

Mocassin imetayarishwa na Daz Naledge, producer wa muziki kutoka Tanzania ambaye pia alihusika kutayarisha Currebt Situation Ya Country Wizzy na Young Lunya

Leave your comment