Chino Kidd Afichua Jinsi Alivyomsaidia Harmonize Kurekodi Kabla Ya Kuingia WCB Wasafi

Image Source: Online

Writer: Charles Maganga 

Msanii na dansa maarufu kutoka Tanzania, Chino Kidd hivi karibuni amefichua jinsi ambavyo alihusika kumsaidia Harmonize kabla hajaingia WCB Wasafi.

Chino Kidd ameyasema hayo hivi karibuni wakati yupo kwenye mahojiano ambapo alidokeza kuwa kuwa yeye ndiye alimfanyia urahisi Harmonize kurekodi wimbo wake wa kwanza ndani ya studio za Mazuu Records. 

Chino anasema kuwa wakati anatafuta nafasi, Harmonize alikuwa anaishia nje studio lakini yeye alimpambania mpaka akapata nafasi ya kurekodi nyimbo mbili kwa Mazuu ambazo ni "Kidonda Changu" na "Aiyola" nyimbo ambazo ndizo nyimbo zilizomtambulisha kimuziki

"My Brother Harmonize mimi ndiye niliyemuingiza pale Mazuu Records ambapo akakutana na Maxmizer na ndipo akafanya ile ngoma ya nini ile Kidonda Changu na Aiyola" 

Chino Kidd aliongeza kuwa aliweza kumunganisha Harmonize kwa sababu Maxmizer alikuwa ni rafiki yake katika kipindi hicho ambacho alikuwa ni dancer wa msanii Rich Mavoko.

Leave your comment