Hawa Ndio Wasanii Walioshirikishwa Kwenye "Therapy" Albamu Mpya Ya Jay Melody

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Zikiwa zimebakia siku chache tangu Jay Melody aachie albamu yake ya kuitwa Therapy, tayari msanii huyo ameachia tracklist ya albamu hiyo.

Jay Melody alitangaza kuachia albamu yake ya kwanza Ijumaa hii ya Tarehe 26 Aprili ambapo albamu hiyo iliyopewa jina la "Therapy" inatarajiwa kuwa albamu ya kwanza ya Jay Melody tangu aanze muziki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jay Melody hivi karibuni aliweka chapisho linaloonesha kuwa albamu ya Therapy itakuwa na ngoma 12.

Wasanii watakaoshirikishwa ni pamoja na Marissa, Karma, Ndelah Magic, Logic na Benson Hauzimi ambao watasikika kwenye ngoma ya kwanza ya kuitwa "Bado" wakati msanii Phina atasikika kwenye ngoma ya kuitwa "Usiniache"

"Therapy" inakuwa ni albamu ya kwanza kuingia sokoni kwa mwaka huu kutoka kwa msanii wa Bongo Fleva.

Leave your comment