Jay Melody Afichua Jina Na Tarehe Ya Kuachia Albamu Yake Mpya

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Msanii nguli kutoka Tanzania, Jay Melody hivi karibuni ametangaza jina pamoja na tarehe ambayo anatarajia kuachia albamu yake ya kwanza tangu aanze muziki.

Jay Melody amedokeza kuhusu ujio wa album yake kupitia ukurasa wake wa Instagram huku taarifa hiyo ya albamu ikiwa inakuja takriban miezi mitatu tangu msanii huyo aachie ngoma yake ya "Baridi"

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jay Melody alidokeza kuwa album yake ya kwanza itaitwa Therapy na inatarajiwa kuingia sokoni Aprili 26 mwaka huu wa 2024.

Ikumbukwe kuwa tangu aanze kufanya muziki rasmi mwaka 2017, Jay Melody hakuwahi kuachia EP au albamu yoyote, hivyo ujio wa albamu hii umezua shangwe kubwa baina ya mashabiki zake.

Leave your comment