Obby Alpha Aachia Ngoma Mpya 'Nimewasamehe'

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Msanii nguli wa Injili kutoka Tanzania, Obby Alpha hivi karibuni ameamua kukata kiu ya mashabiki zake baada ya kuachia wimbo mpya wa kuitwa 'Nimewasamehe'

Kwenye 'Nimewasamehe' Obby Alpha anazungumza na watesi wake akiwakumbusha kuwa amewasamehe kwa njia yoyote waliyomkosea huku akimuomba Mungu ampe neema ya kuweza kuwaachilia.

Uandishi wa Obby Alpha kwenye wimbo huu ni wa kiwango cha juu ambapo humu ndani, Obby ameongeza vionjo vya Tanzanian Gospel na muziki Bongo Fleva kwa mbali.

Aidha 'Nimewasamehe' ni ngoma ya kwanza ya Obby Alpha kwa mwaka huu wa 2024, ikiwa pia ni miezi michache tangu aachie 'Bora Kushukuru'

https://youtu.be/HihLCDVi8ms?si=AKTmOvFKiKPBtSRY

Leave your comment