Tanzania Music Awards 2024 Kurushwa Live Kupitia Chaneli Ya MTV Base Na BET

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Baada ya kuwa na msimu mzuri mwaka jana, waandaaji wa tuzo za muziki Tanzania maarufu kama Tanzania Music Awards hivi karibuni wametangaza kuwa kwa msimu wa 2024 tuzo hizo zitaoneshwa kwenye vituo vya BET na MTV BASE.

Tangazo hilo lililozua shangwe baina ya wapenzi wa burudani Tanzania lilitolewa hivi karibuni kupitia vyombo vya habari.

Mwanakamati wa Tanzania Music Awards 2024, Seven Mosha ambaye pia ni CEO wa lebo ya Rockstar alidokeza kuwa kwa mara ya kwanza tuzo hizo zitaoneshwa kwenye vituo hivyo.

"Na ya tano ambayo kamati tunaweza kusema we're very proud of ni kwamba tuzo hizi the international media ambayo itai-cover ni MTV na BET" alizungumza Seven

Ushirikiano baina ya Tanzania Music Awards na MTV pamoja na BET unakuwa ni ushirikiano wa kwanza wa aina yake barani Afrika.

Leave your comment