Hanstone Afichua Chanzo Cha Kuachana Na WCB Wasafi

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Kama kwa muda mrefu ulikuwa ukisubiri kufahamu chanzo cha Hanstone, msanii nguli wa Bongo Fleva kuachana na WCB Wassfi basi msanii huyo hivi karibuni amefunguka kuhusu sakata hilo.

Taarifa za Hanstone kuondoka Wasafi zilianza mwaka 2022 ambapo hivi karibuni msanii huyo alithibitisha kuwa kipindi kweye lebo hiyo pia alihusika kuandika ngoma tofauti tofauti za wasanii wa WCB Wasafi.

Kwenye mahojiano yake na kituo cha Clouds FM, Hanstone alidokeza kuwa aliondoka Wasafi kwa sababu alikosa amani na pia kwa sababubya kukosa kipato cha kukidhi mahitaji yake kipindi anasubiria kutambulishwa.

"Kuna vitu tu naweza kusema haviko kwenye love, vinaweza vikakufanya usiishi na amani. Alafu mi napenda sana amani kwenye maisha yangu. Kwa hiyo pale (Wasafi) kuna kitu nilikuwa nashindwa kupata" alizungumza Hanstone

Leave your comment