Harmonize Atamba Kuwaburuza Rayvanny Na Diamond Platnumz

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Ushindani kwenye soko la muziki nchini Tanzania umeendelea kuwa wa moto na hii ni baada ya msanii Harmonize kutamba kuwaburuza wasanii wenzake, Rayvanny na Diamond Platnumz.

 

Harmonize ametoa tambo hizo hivi karibuni mara baada ya Charts Tanzania kutoa orodha ya ngoma ambazo zimesikilizwa zaidi kwenyw mtandao wa Spotify kwa muda wote.

Katika orodha hiyo, "Tetema" ya Rayvanny ilikaa namba moja, ikifuatiwa na Commando ya Mavokali, African Beauty na Inama za Diamond Platnumz huku Single Again ikikaa kwenye nafasi ya 5.

Harmonize alitumia ukurasa wake wa Instagram upande wa Instastory ambapo mkali huyo wa Bongo Fleva kuandika kuwa wimbo wake wa Single Again ndio ngoma bora ya mwaka 2023 kwani ndio wimbo pekee kwenye orodha hiyo ambao umetoka mwaka jana na kwamba ngoma nyingine zote ni za zamani

"Haya watoa tuzo nadhani mshaelewa ipi ni ngoma kubwa 2023 maana wamepost mwenyewe leo. Nyingine zote za zamani" aliandika Harmonize

"Single Again" ni ngoma ya Harmonize ambayo ilitoka mwanzoni mwa mwaka 2023 na iliweza kuvuka mipaka na kuwa moja ya ngoma kubwa Afrika

Leave your comment