"Nilisainiwa Wasafi 2019" Hanstone Afunguka

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga

Baada ya ukimya wa muda mrefu hatimaye msanii na mwandishi mahiri kutoka kwenye kiwanda cha Bongo Fleva, Hanstone hivi karibuni amefunguka kuhusu sakata la yeye kusainiwa kwenye lebo ya WCB Wasafi. 

Hanstone kwa muda mrefu sasa alihusishwa kusainiwa kwenye lebo ya Wasafi ambapo takriban miezi michache nyuma taarifa kupitia vyombo vya habari ziliripoti kuwa msanii huyo ameachana na lebo hiyo. 

Akiwa kwenye mahojiano hivi karibuni Hanstone alithibitisha kuwa alisainiwa Wasafi mwaka 2019 na alidumu kwenye lebo hiyo kwa takriban miaka 3 akisubiri kutambulishwa rasmi. 

"Nakumbuka 2019 (kusainiwa). Haikuwa mpaka yani we ndo ushasainiwa hapo subiria utatoka lini. Sasa kuna vitu mi niliishi mwaka wa kwanza, wa pili wa tatu mi ndo nikaondoka pale." alizungumza Hanstone 

Kabla ya kuingia Wasafi, Hanstone alikuwa akifanya kazi kkwa ukaribu na Abbah Process na pia msanii huyo alishirikiana na Maua Sama kwenye ngoma ya "Iokote"

Leave your comment