Ngoma Mpya: Ruby Na Kusah Waungana Kwenye "Leo"

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Msanii kutokea lebo ya Majeshi Music Ruby ameamua kuburudisha mashabiki na kibao kipya cha "Leo" ambacho amemshirikisha Kusah.

Ruby alidokeza kuhusu ngoma hii siku chache nyuma na hivyo kusababisha hari baina ya mashabiki hasa ukizingatia kuwa wawili hao licha ya kuwa wasanii wa Bongo Fleva pia ni wazazi wenza.

"Leo" ni ngoma yenye miondoko ya Bongo Fleva ambayo ndani yake Ruby, anaimbia na kutoa somo kwa watu wanaopenda kufuatilia husiano lake na mpenzi wake.

 

Mkali wa "I Wish" Kusah alipamba ngoma hii kwa sauti ya mujarab na kufanya mradi huu mzima uwe na sifa ya kusikilizika zaidi ya mara moja.

Ngoma ya "Leo" imetayarishwa na fundi wa muziki kutoka Tanzania, Fraga ambaye pia ni msanii wa muziki

https://youtu.be/TmWdwAda27w?si=jLU4Ixq0CG3x9D8r

 

Leave your comment