Young Lunya Na Diamond Platnumz Wadokeza Ujio Wa Ngoma Mpya

Image Source: Online

Writer: Charles Maganga 

Huenda wakali wawili wa Bongo Fleva Diamond Platnumz na Young Lunya wakaachia ngoma ya pamoja hivi karibuni na hii ni kutokana na kionjo alichoachia Young Lunya hivi karibuni.

Baada ya ukimya wa muda mrefu, Young Lunya hivi karibuni Young Lunya amedokeza ujio wake mpya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Young Lunya aliweka kionjo cha ngoma yake mpya ambayo katika video hiyo Lunya alionekana akiwa na S2kizzy studio na kuandika "Verse Yako Iko Wapi", swali ambalo Diamond alilijibu kwa kudokeza kuwa atakamilisha verse hiyo usiku wa leo.

Young Lunya kwa sasa yuko chini ya Rockstar Africa na ana CV ya kufanya kazi na wasanii tofauti tofauti wakubwa kutoka Tanzania kama Country Wizzy, Mimi Mars, Msamiati na wengine kibao

Leave your comment