Watanzania Wengine Washiriki Kwenye 'American Got Talent'

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Kama ulifurahi na kushabikia kundi la Ramadhani Brothers kushinda America's Got Talent basi habari njema ni kwamba kundi jingine kutoka Tanzania limetangaza kushiriki mashindano hayo.

Kundi la wanasarakasi, la kuitwa Hakuna Matata Acrobats limetangaza kuwa litashiriki kwenye mashindano ya mwaka huu ya America's Got Talent katika msimu wa 19. 

Kundi hilo la Hakuna Matata wataungana na Ramadhani Brothers kama Watanzania pekee kuwahi kushiriki kwenye shindano hilo. 

Hakuna Matata Acrobats liliundwa mwaka 2003 na Winston Ruddle, ambaye ni mwalimu na meneja wa Ramadhani Brothers.

Msimu mpya wa America's Got Talent utaanza kuoneshwa kupitia kituo cha runinga cha NBC Mei 28, 2024, na episodes zitarushwa kila wiki hadi Agosti 13, ambapo baada ya hapo live shows zitaanza kurushwa. Mshindi wa AGT ataibuka na kitita cha dola milioni 1 za Marekani, ambazo ni takriban shilingi bilioni 2.6 za Tanzania.

Leave your comment