Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Stamina Afichua Marapa Wawili Kutoka Kenya Aliowashirikisha Kwenye Albamu Yake Inayotarajiwa Kuachiwa Hivi Karibuni
3 April 2024

Image Source: Online
Writer: Charles Maganga
Wakati wapenzi wa muziki Tanzania wakisubiri kwa hamu albamu ya rapa Stamina, msanii huyo hivi karibuni amewataja wasanii wawili kutoka Kenya watakaoshiriki kwenye albamu hiyo.
Akiwa kwenye mahojiano hivi karibuni, Stamina alidokeza kuwa King Kaka na Meja watakuwepo kwenye albamu yake ambayo inatarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni
"Wapo wengi sana. Wapo kina Meja Kenya, King Kaka na wengine sikutajii kwa sababu kuna wengine kutoka Rwanda. Kuna Ufaransa. Nna watu wengi" alizungumza Stamina.
Kufikia sasa bado Stamina hajaweka wazi jina la albamu hiyo, jumla ya ngoma zitakazokuwepo au hata tarehe ambayo albamu hiyo litaingia sokoni.
Weekly Top 10 songs
Top stories
- Diso Ziod
21 April
- Lesson
20 April
- Drop new song loyo
21 April




Leave your comment